LIWAKA AMGARAGAZA MASALA KURA ZA MAONI UBUNGE LA NACHINGWEA

 

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Fadhili Liwaka ameongoza kura 4703 za wajumbe jimbo la Nachingwea za kuomba ridhaa ya kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge wa jimbo hilo.

Mpinzani wake mkubwa, Hassan Massala amefuatia kwa kuwa na kura 3307.

Jumla ya kura zote: 11978

Kura halali zilizopigwa: 9471

FADHILI ALLY LIWAKA 4703

HASSAN ELIAS MASALA – 3307

AMANDUSI CHINGUILE – 599

MAIMUNA PATHAN – 428

MOHAMEDI UNGELE – 338

ISSA MKALINGA – 116

Tofauti ya kura Kati ya LIWAKA na MASALA ni kura 1396.