Wahi Kwa Mkapa uione Taifa Stars bure

CHAN 2024 inaendelea leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, grupu B likicheza mechi zake za pili.

Mchezo wa mapema utapigwa kuanzia saa 11:00 Jioni ukizihusisha timu za Taifa za Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati huku mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Mauritania ukitarajiwa kuanza saa 2:00 usiku.

Kupitia ukurasa rasmi wa Shirikisho la soka Tanzania TFF limechapisha habari njema kwa mashabiki 10000 wa kwanza wa Mzunguko kuingia bure kutazama mchezo huo.

“Wanetu wa Mzunguko watu 10,000 wa kwanza mnapata ofa ya tiketi ya kuingia uwanjani bila kulipa, unachotakiwa kufanya beba Kadi yako ya N Card suala la tiketi ya kuingia tuachie sisi, utaangalia mechi zote mbili”

Aidha Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa, Neema Msitha, amesema Watanzania watakaofika leo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa watapata nafasi ya kutazama mechi mbili kwa kiingilio kimoja katika mchezo utakaochezwa majira ya saa 11:00 jioni na ule wa saa 2: 00 usiku.

Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars ilishinda dhidi ya Burkinafaso kwa mabao 2-0.