……………
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Octoba 29 Mwaka huu ,Viongozi wa vya Siasa walioko Jimbo la Uchaguzi Vijijini wakutana kujadili Ratiba ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.
kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi wa vyama vya Siasa, Viongozi wa dini na Vyombo vya ulinzi na Usalama.
Vyama vya Siasa vilivyoshiriki Kikao hicho ni pamoja na Chamma Cha Kijamii (CCK), CUF, NCCR- Mageuzi’ Chama Cha Sauti ya Umma ( SAU), CHAUMA, UDPP, ACT-Wazalendo na Chama cha Mapinduzi( CCM).
Akizungumza katika kikao hicho Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kibaha Vijijini Bi Tukelage Kidenya amewataka viongozi wa Vyama vya Siasa kusoma na kuelekea Maelekezo ya Uchaguzi kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili Kuepusha Malalamiko Wakati wa Uchaguzi na Baada ya Uchaguzi.
Bi Kidenya alipata fursa ya kuwasomea ratiba kuelekea Uchaguzi Mkuu katika Hatua mbalimbali ikiwemo uteuzi wa wagombea na ratiba ya Kampeni.
Pia Bi Kidenya aliwataka Viongozi wa vyama vya Siasa kufanya Kampeni za kistaarabu, zisizo na Lugha chafu, matusi na kejeli zinazoathiri utu wa mwingine.
Ambapo viongozi wa Vyama vya Siasa Wamekubaliana Kwa pamoja Kupeleka majina ya wagombea wao Wa Ubunge na Udiwani⁷ kabla ya Agosti 27 mwaka huu.
Kwa upande wake Afisa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Bi Grace Haule amewataka viongozi wa Vyama vya Siasa kuandaa ratiba ya Kampeni ya vyama vyao ambayo haitakuwa na mgongano wakati wa Kampeni na baadaye kupata ratiba kuu itakayotumika wakati huo wa Kampeni utakapofika.
Hii itasaidia kuepusha Migogoro na kuleta Amani na utulivu katika kipindi chote cha Kampeni, ambapo Kampeni zitaanza rasmi tarehe 28Agosti hadi 28 Octoba Mwaka huu.
Kwa nyakati tofauti viongozi wa Vyama Siasa na viongozi wa dini wamepongeza hatua hiyo kwani ni ishara tosha ya uwazi, uhuru na haki Kwa vyama vyote vya Siasa.
Hivyo wameahidi kufuata Maelekezo ya Uchaguzi yaliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania na kufanya Kampeni za kistaarabu wakati Wote Wa Kampeni utakapofika.