Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo tarehe 12 Agosti, 2025 amekabidhi fomu ya uteuzi kwa mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kutoka Chama cha Kijamii (CCK), David Daud Mwaijojele akiwa ameambatana na mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais kwa tiketi ya Chama hicho, Mhe. Masoud Ali Abdala katika Hafla hiyo ambayo imefanyika kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma.
………………….
CHAMA Cha Kijamii (CCK)
kimesema kuwa kikifanikiwa kushika dola watahakikisha wanaboresha maisha bora na
kuongeza ajira kwa watanzania wakiwemo waandishi wa habari na wastaafu.
Mgombea wa Kiti cha
Rais wa Jamhuri ya Muungano kutoka Chama cha Kijamii (CCK), David Daud Mwaijojele
wakati alipokabidhiwa fomu ya uteuzi wa
nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa tume hiyo,
Jaji Mstaafu Jacobs Mwambegele kwenye Ofisi za Makao Makuu ya tume hiyo
zilizopo Njedengwa mkoani Dodoma akiongozana na Mgombea Mwenza wa nafasi ya
Makamu wa Rais, Masoid Ali Abdalla.
Amesema serikali ya CCK
itakapopewa ridhaa na wananchi wanatawajengea nyumba wastaafu ili waweze
kuyafaidi maisha