Morocco haitaki kurudia makosa CHAN 2024

KOCHA wa Morocco, Tarik Sektioui amesema makosa waliyoyafanya kwenye mechi iliyopita dhidi ya Kenya wanayafanyia kazi ili kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Zambia.

Agosti 10, Morocco ilipoteza bao 1-0 dhidi ya Kenya, ikiwa ni mchezo wao wa pili kwenye Kundi A. Mechi ya kwanza walishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Angola, na kuwafanya Waarabu hao kuwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi.

Kesho  Alhamisi, Morocco wataikaribisha Zambia Uwanja uliopo mkiani na kocha huyo alisema haitarudia makosa waliyofanya kwenye mechi iliyopita waliyopoteza nafasi nyingi.

“Wakati mwingine si rahisi kabisa, lakini nafikiri tuliianza mchezo vizuri na tulifanya maamuzi mengi mazuri tulidhibiti mchezo mwanzoni, lakini baadaye, nafikiri tulienda kwa mapitio mengi na udhibiti ambao haukuwa mzuri. Hatukuwa wazuri kiufundi,” alisema.

“Tulikosa nafasi nyingi katika nusu ya kwanza, na katika ya pili, tukiwa na faida ya mchezaji mmoja zaidi, hatukufanya bora kabisa.”

“Hayo yameisha na kwa sasa tunajiandaa na mechi dhidi ya Zambia. Sio mpinzani rahisi na tutafanyia kazi uchezaji wa timu zinazozuia vizuri ili kuvuka hatua zinazofuata.”

Bado kundi hilo, kila timu ina nafasi ya kuvuka kwenda robo fainali, ambapo Morocco inahitaji pointi sita kwenye mechi mbili zilizosalia dhidi ya Zambia na Congo, wakati Kenya inahitaji pointi tatu kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Zambia.