Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Dkt Debora Magiligimba ambaye pia ni mratibu wa shughuli za Shirikisho la polisi wanawake duniani IAWP ( International Association of Women Police) wa ukanda wa 21 Southern Africa countries na Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya shirikisho la Polisi wanawake duniani ameongezewa majukum ya kuratibu shughuli za IAWP Kwa ukanda wa 20 -Eastern Africa countries wenye jumla ya nchi 14.
SACP Dkt Magiligimba alikuwa Mratibu wa shughuli za IAWP ukanda wa 21 – Region 21 Coordinator ,wenye jumla nchi 11 ambapo kwa sasa ni mratibu wa shughuli za IAWP jumla ya nchi 25 zilizoko bara la Afrika. Yaani Kwa sasa ni IAWP Region 21 Coordinator for the united Region 20 and 21.
Nchi ambazo ataziongoza chini ya Mwamvuli wa Shirikisho la polisi wanawake duniani ni ukanda wa 20 wenye nchi 14 zilizoko Eastern Africa ambazo ni- Burundi, Comoros, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mayotte, ReunionIsland, Rwanda, Seychelles, Somalia, South Sudan, Uganda pamoja na ukanda wa 21 wenye nchi zilizoko Southern Africa ambazo ni – Angola, Botswana, Lesotho, Malawi, Mozambique, Namibia, South Africa, Swaziland, Tanzania, Zambia, Zimbabwe
Aidha hii ni heshima kubwa kwa SACP Dkt. Magiligimba, ambaye sasa ataendelea kuiwakilisha vyema Tanzania katika majukumu yake katika shirikisho la polisi wanawake (IAWP ) inayolenga kukuza haki, usawa wa kijinsia na kuwajengea uwezo wa kiutendaji polisi wanawake na wanawake wangine wanaofanya kazi katika vyombo vingine/ taasisi zingine za utekelezaji wa Sheria duniani Kote.
Uteuzi wake ni ishara ya imani kubwa kwa uwezo wake Mkubwa kiutendaji katika nyanja ya Utawala, kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na kusimamia usawa wa kijinsia katika shirikisho hilo la polisi wanawake duniani. IAWP
Uteuzi huo umefanywa na rais wa Shirikisho la polisi wanawake duniani Bi Julia Jaeger wa UK.