UDP WATAMBA NA SERA YA KUWAJAZA MAPESA WANANCHI, HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UONGOZI


Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

CHAMA cha United,Democratics Party,(UDP) kimesema kama kitapewa ridhaa ya kushika dola kitawajaza watanzania fedha ili waweze kujikomboa kiuchumi,huku wakikisisitiza suala la haki za wanawake katika uongozi ikiwemo kutokomeza ukatili wa kijinsia.


Hayo yamesemwa leo Agosti 15,2025 na mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama hicho,Saum Hussein Rashid wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma,mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) iliopo Njedengwa Dodoma

Saum akiwa na mgombea mwenza,Juma Khamisi Faki,amesema watawajaza fedha watanzania kwa kufungua fursa mbalimbali katika sekta za kilimo,kuboresha miundombinu pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu katika sekta ya elimu.

“Tunaposema kuwajaza fedha watanzania tuna maana ni kuweka miundombinu mizuri kwa wananchi ili waweze kupata fedha ambazo zitawainua kiuchumi kwa mfano zao la Pamba walime kisasa na mazao mengine.

Amesema pia ni kuboresha ile miundombinu ya watu kuwa na fedha kwa sababu atafanya kilimo chenye tija ndio maana tunasema kuwajaza fedha ni kufungua fursa zinazopelekea biashara kufanyika.

Kuhusu suala la haki ya wanawake katika uongozi amesema UDP itahakikisha wanawake wanaingia katika uongozi na kuongeza watatokomeza pia ukatili wa kijinsia.

 

Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Party (UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid akiwa na Mgombea Mwenza, Mhe. Juma Khamis Faki (kushoto) wakionesha beki la fomu za uteuzi walililokabidhiwa na Tume.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Party (UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Juma Khamis Faki (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 15, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima.  (Picha na INEC).



Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Party (UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid akielekezwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ndg Ramadhani Kailima namna ya kusaini kitabu.

Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Party (UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid akielekezwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ndg Ramadhani Kailima namna ya kusaini kitabu.

Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Party (UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid akisaini kitabu.
Mgombea Mwenza, Mhe. Juma Khamis Faki akisaini kitabu.


Wajumbe wa Tume wakiwa katika utoaji fomu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza wakati wa utoaji fomu za uteuzi kwa wagombea wa Chama cha UDP.
Wagombea wa Chama cha UDP wakiwa ukumbini.

Baadhi ya wanachama wa UDP wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu.


Baadhi ya wanachama wa UDP wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu.

Baadhi ya wanachama wa UDP wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu. 


Baadhi ya wanachama wa UDP wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu. 



Mgombea wa UDP akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu.