Dar es Salaam. Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin, wamatarajia kukutana leo huko Alaska katika mkutano wa kihistoria wa majadiliano ya vita imayoendelea kati ya Russia na Ukraine.
Mkutano huo utakuwa mjini Anchorage, Alaska saa 5:30 asubuhi kwa saa za huko (saa 11:30 jioni EAT).
Trump amesema anaamini Putin anataka kufanya makubaliano ya kumaliza vita vya Ukraine, lakini akatahadharisha kuwa kuna uwezekano wa asilimia 25 mkutano usifantyike.
Kwa mujibu wa CNN Trump ameitishia Russia endapo Rais Putin hatakubali kumaliza vita ikiwa mkutano huo utafanikiwa.
Hata hivyo, Trump amependekeza kuandaa kikao cha pande tatu na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambacho kinaweza kujumuisha viongozi wa Ulaya.
Kwa upande wake Putin amepongeza juhudi za serikali ya Trump za kusitisha vita na kuashiria kuwa Moscow na Washington zinaweza kufikia makubaliano ya kudhibiti silaha za nyuklia katika mkutano huo.
Putin ametoa kauli hiyo wakati alipozungumza na mawaziri waandamizi na maofisa wa usalama wakati akijiandaa kukutana na Trump hii leo jimboni Alaska.
Imeelezwaakubaliano ya amani yatategemea makubaliano ya maeneo, ambapo Urusi inashikilia takriban sehemu ya tano ya ardhi ya Ukraine.
Trump amesema anaamimi mkutano unawez kuwa mzuri au mbaya utaisha haraka. Kama ni mzuri, tutapata amani hivi karibuni. Amesema.
Trump pia amerudia kauli yake kwamba uvamizi wa Ukraine usingetokea kama yeye angekuwa Rais tangu awali, akidai kuwa Putin “asingethubutu.”
Russia iliivamia Ukraine Februari 24, 2022 ambapo kumeemdelea kiwepo mapigano yanayopasua vichwa vya viongozi wakuu wa kidunia namna ya kuyamaliza.
Ingawa Viongozi wa Ulaya, wakiwemo Zelensky, wameachwa nje ya majadiliano haya awali walifanya mkutano wa mtandaoni na Trump ili kuwasilisha msimamo wao.