Sauti ya mgombea yapotea, akomaa kuomba kura

Katika hali ya kushangaza, mgombea wa kanda namba tatu, James Mhagama amepata changamoto ya sauti ambayo imemfanya ashindwe kusikika vizuri.

Kabla ya kuomba kura, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Kiomoni Kibamba amewajulisha wajumbe kuwa Mhagama amepata chagamoto ya sauti.

“Jana alikuwa anasikika vizuri lakini leo ana changamoto kidogo sasa sijui ni mambo ya kiuchaguzi,” amesema Kibamba na kufanya wajumbe waangue kicheko.

Hata hivyo, Mhagama pamoja na sauti yake kuwa ya chini bado ametumia nafasi yake kuomba kura.

Uchaguzi wa TFF unafanyika muda huu jijini Tanga ambapo tayari Rais Wallace Karia ameshapita kuongoza tena shirikisho hilo kwa kipindi cha mwisho cha miaka minne.