TAASISI YA BAOBAB YASHIRIKISHA SHULE 12 ZA SEKONDARI BAGAMOYO KUKUZA MICHEZO

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika  suala zima la kuboresha sekta ya michezo uongozi wa  shule ya sekondari Baobab pamoja na chuo cha afya  cha Bihas vilivyopo  Kata ya Mapinga Wilaya ya Bagamoyo imeamua kufanya bonanza kubwa la michezo ambalo limeshirkisha jumla ya  shule 12 za sekondari  lengo ikiwa ni kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi wa kike na wakiume.

Bonanza hilo ambalo limehudhuliwa na viongozi  wa serikaali, walimu kutoka shule mbali mbali, wadau wa michezo pamoja na wanafunzi kutoka maeneo mengine ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo washindi katika mchezo wa soka wameweza kuzawadia zawadi mbali mbali ikiwemo kupatiwa vikombe  pamoja na  medali ikiwa pamoja na wale wanafunzi wa kidato cha sita ambao wamefanya vizuri katika taaluma.

Akizungumza wakati wa halfa ya bonanza hilo Afisa taaluma wa Halmshauri ya Wilay ya Bamoyo Juma Selemani  ambaye pia aliyekuwa  ni mgeni rasmi  katika shughuli hiyo amewapongeza kwa dhati viongozi wa Taasisi ya Baobab kwa kuweza kuamua kukuza  na kuibua vipaji vya wanafunzi kupitia bonanza hilo ambalo limeweza kuwa la kihistoria kutokana  na mwamko kuwa ni mkubwa.

Amebainisha kwamba katika bonanza hilo ameweza kubaini kuwepo kwa vipaji mbali mbali kutoka kwa wanafunzi wa kike na wakiume katika mchezo wa soka sambaambaa na vipaji na uwezo mkubwa katika mashindano ya kitaaluma ambayo yameweza kuonyeshwa na wanafunzi mbali mbali.

“Napenda kutoa pongezi kubwa kwa uongozi mzim wa taasisi ya Baobab ambaapo leo tumeweza kushuhudia bonanza ili kubwa ambalo limeambatanaa na michezo mbali mbali pamoja na uzinduzi wa chuo cha afya naa sisi kama serikali tutaaendeleaa kushirikiaanaa beg kwa bega kwa lengo la kuwez kuleta maatokeo chaanyaa katika sualaa laa kukuza taalumu pamoja naa kukuza vipaaji kwa wanafunzi,”amebainisha Suleman.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa  taasisi hiyo ya Baobab  Shani Swai  amesema kwamba  lengo lao kubwa ni kuendelea kukuza michezo na kwamba watajitahidi sana  kuhakikisha wanajenga mazingira rafiki  kwa lengo kuwawezesha wanafunzi waweze kucheza viwanjaa vyenye ubora ambao unatakiwa.

Naye Mkuu wa chuo cha afya cha Baobab Nelsen Rahul amebainisha kwamba dhumuni la bonanza hilo ni kuendelea kuwashirikisha watu mbali mbali wakiwemo wanafunzi pamoja na watoto wenye ulemavu kwani michezo na kwamba mikakati  yao ni kuendeleza kufanya mabonanza zaidi kwa lengo la kukuza vipaji na kuimarisha afya.

Katika bonanza  hilo ambalo limeweza kugonga nyoyo za wanafunzi  timu ya shule ya sekondari  Shushila  wameweza kubuka na mabingwa  wa jumla  baada  ya kuwachapa wapinzani wao  wenyeji wa  shule ya Sekondari Baobao kwa bao 1-0 katika mchezo mkaali uliokuwa wa vuta ni kuvute kutokana ana wachezaji wote kuonyesha vipaji vya hali ya juu.

Baadhi ya shule za sekondari ambazo zimeweza kupata fursa ya kipekee katikaa kushiriki katika Bonanza hilo ni pamojaa na wenyeji shule y Sekondari Baobab,Dunda Sekondari, Mapinga, Dunda, Nia njema,Kerege, Kingani, Fukayosi.