:::::::::
Chini ya Rais Samia, mapato ya ndani yameongezeka kutoka shilingi trilioni
20.59 mwaka 2020|21 (wastani wa trilioni 1.72 kwa mwezi) hadi trilioni 29.83
mwaka 2023|24 (wastani wa trilioni 2.49 kwa mwezi) kwa sasa mapato
yamefikia trilioni 3 kwa mwezi, huku kati ya Julai 2024 hadi Mei 2025
yakipanda zaidi kufikia wastani wa trilioni 2.83 kwa mwezi.
Vilevile, uwiano
wa mapato ya ndani kwa Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 13.7
mwaka 2020/21 hadi asilimia 15.0 mwaka 2023|24, hali inayoonesha
mageuzi makubwa na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.