Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
MGOMBEA Udiwani kata ya Kibosho kati Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi kupitia chama cha Mapinduzi, Bahati Mamboma amechukua fomu ya kuwania kiti hicho katika Ofisi ya Mtendaji kata.
Mambo ambaye alisindikizwa na wanachama na CCM pamoja na wananchi wa kata hiyo alitumia nafasi hiyo kuwaahidi wananchi endapo watamchagua kwa kipindi kingine atahakikisha anaendeleza kazi zote alizokuwa amekwisha zianza katika kipindi kilichopita.
Pia aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha kata hiyo inazidi kupiga hatua katika maendeleo.