KOCHA Mkuu wa Senegal, Souleymane Diallo amelia na kikosi chake kushindwana kutegua mtego dhidi ya Sudan akisisitiza kuwa ana kazi kubwa ya kufanya katika hatua ya robo fainali akihofia kukamiwa zaidi.
Souleymane alisema hayo baada ya timu yake kuambulia suluhu dhidi ya Sudan akikiri kupata mchezo mgumu ambao uliifanya timu yake ishindwe kupata matokeo kucha ya kucheza vizuri kutokana na mbinu iliyowalipa wapinzani wake ya kuzuia zaidi.
“Licha ya kujaribu mbinu zote nikifanya mabadiliko ya wachezaji watato bado tulishindwa kuharibu mbinu za mpinzani wetu alikuwa imara sana kwenye maeneo mengi ukiacha ukuta wao uliokuwa imara zaidi,” alisema na kuongeza:
“Tumefuzu lakini naweza kusema tumekutana na ugumu hii ni kutokana na picha iliyopo kwa wapinzani kwamba wanacheza na bingwa mtetezi tuna kazi ya kufanya ilo tuwe bora zaidi nina kikosi kizuri nahitaji kuwa na mbinu zaidi ili kuweza kutetea taji.”
Alisema hatua inayofuata wanatarajia ushindani zaidi wao kama mabingwa watetezi watahakikisha wanakuwa bora na kuheshimu kila mpinzani ili kujiondoa kwenye mtego wao wa kishikilia taji la michuano hiyo.
Senegal ndio watetezi wa michuano hiyo baada ya kuchukua taji hilo mwaka 2022, ilipowafunga wenyeji Algeria kwa penalti 5-4, kufuatia suluhu ya (0-0) katika dakika 120.