Klabu ya Azam FC imeachana rasmi na kipa wake raia wa Sudan, Mohamed Mustafa, baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Azam FC imetoa ujumbe maalumu kuthibitisha kuachana huko, ikibainisha kuwa uhusiano huo umehitimishwa kwa amani na kwa heshima baina ya pande zote.
Mustafa, ambaye alijiunga na Azam FC akitokea soka la Sudan, amehudumu klabuni hapo katika kipindi ambacho kilionekana kuwa cha mabadiliko kwenye safu ya ulinzi wa lango la timu hiyo.
Kwa sasa Azam FC inaendelea na maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa mashindano, huku safari ya Mustafa ikibakia kuwa sehemu ya historia ya klabu hiyo ya Chamazi.