RC CHALAMILA AZINDUA MFUMO WA USAMBAZAJI GAS YA ORYX KATIKA SOKO LA FERRY

 :::::::::

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo Agosti 21 amezindua mfumo wa kwanza wa usambazaji wa gas ya LPG kwa wingi katika soko la Samaki la kimataifa la Ferry Jijini Dar es Salaam mradi ambao umetekelezwa na KAMPUNI ya ORYX Energies Tanzania kwa kushirikiana na Serikali.

Mradi huo wa kihistoria ni hatua kubwa katika kuimarisha upatikanaji wa nishati safi kwa wauzaji wa samaki na wajasiriamali wadogo katika soko hilo ambapo sasa mfumo huo unaweza kulipia kadri ya matumizi (PAYG), unaowawezesha wauzaji kulipia gesi wanayotumia tu na hivyo kuondoa gharama kubwa za kujaza mitungi na kupunguza matumizi ya kila siku hadi Sh.45,000.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo huo ambapo limejengwa tanki kubwa ambalo linatumika kusambaza gesi katika majiko ya wafanyabiashara hao, RC Chalamila amesema mfumo huo sasa utawezesha kulipa kulingana na matumizi yako pia mfanyabiashara sasa ana mita yake inayosoma matumizi yake ya kila siku, kabla na baada ya matumizi, hakuna tena kubahatisha, hakuna tena kulazimika kununua mitungi midogo kwa gharama kubwa, vilevile Oryx wamezingatia usalama, kwa kufunga valve ambazo zitatumika kufunga gesi endapo itatokea dharula kwa kila jiko. 

Hata hivyo viwango vya matumizi gesi vitafuatiliwa kwa urahisi ili kuhakikisha gesi inaletwa kujaza kwenye hili tanki kubwa kwa wakati huku akieleza gharama imepungua na wafanyabiashara waliokuwa wakitumia hadi Sh.180,000 kujaza gesi kwa siku sasa wanaweza kuokoa hadi Sh.45,000 kila siku. “Kupitia mfumo wa Lipa Kadri Unavyotumia, hili ni suala la kupongezwa sana, hakuna upotevu, hakuna gesi isiyotumika tofauti na zamani ambapo mtungi mdogo mliotumia wakati fulani gesi inabaki kidogo. Usalama wa Juu, hili sina shaka na utalamu wenu Oryx kwenye suala zima la usalama, nafahamu tahadhari zote zimezingatiwa hasa kwa kuweka Vifaa vya kuzima moto nataratibu za dharura zipo tayari”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Benoit Araman amesema lengo la kuwa na mfumo huo wa kuwa na tanki la gesi katika soko hilo unalenga kupunguza gharama za kujaza, kupunguza upotevu, na kuongeza ufanisi usalama Mfumo usiovuja

Amesema ni mfumo wa kisasa uliofanywa na team ya ufundi ya Oryx gas kwa kuzingatia kanuni za kitaifa na kimataifa, Pia urahisishaji wa Uendeshaji Ugavi endelevu pamoja na ufuatiliaji wa kisasa, na matengenezo madogo.

Awali Katibu Tawala msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Elizabeth Mshote amesma mkakati wa Serikali katika utekelezaji wa ajenda ya Nishati Safi ifikapo 2034 kila wanaposimama watu 10 watu 8 wawe wanatumia Nishati Safi, kwa sasa kila wanaposimama watu 10 watu 3 tu wanatumia Nishati Safi, vilevile takwimu za kitaifa zinasema vifo takribani 33 elfu vinatokea kutokana na madhara ya matumizi ya Nishati chafu, kwa taarifa ya Mkoa katika magonjwa makuu 5 yanayosumbua suala la madhara ya upumuaji ni mojawapo kutokana na Nishati isiyo salama.

Katika hatua nyingine aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Ilala Dar es Salaam Mussa Zungu amesema awali wafanyabiashara wa soko hilo walimfikishia mahitaji yao hivyo aliwatafuta Oryx Gas na leo amefurahi kuona umefungwa mfumo huo ambao unakwenda kurahisisha shughuli za wafanyabiashara hao.

Zungu amesema tafiti zinaonesha duniani kuwa Kuna vifo vingi vinavyotona na Matumizi ya Nishati isio salama hivyo Mradi huu unakwenda kuwa majawabu ya kuimarisha Afya za wadau hao.