Ni robo fainali ya kisasi Ligi ya Kikapu Dar

Ni vita ya kisasi    robo fainali ya Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (BDL) itakayoanza kesho (Jumamosi) kwenye Uwanja wa Donbosco Upanga.

Kila timu inasaka ushindi kwa kulipa kisasi baada ya kufungwa katika hatua ya kwanza ya ligi hiyo na JKT Stars itakutana na Vijana Queens, huku Jeshi Stars itamenyana na  Pazi Queens.

Kwa upande wanaume Dar City itakutana na Srelio, huku Pazi ikitoana jasho na  ABC.

Vijana Queens itataka kulipa kisasi kwa JKT Stars baada ya kufungwa kwa pointi 87-64 mchezo wa kwanza zilipokutana, huku ikijivunia nyota wake Magret Mhonda na Salma Sandali,  waliowapandisha daraja kutoka kikosi cha pili cha City Queens.

Kwa upande wa JKT Stars itakuwa  na Jesca Ngisaise, Sara Budodi, Wade Jaha na Grace Innocent, huku kocha waVijana, Bahati Mgunda akitamba kisasi ni lazima.

Baada ya kichapo cha pointi 80-40 kutoka kwa  Jeshi Stars, Pazi Queens inataka kulipa kisasi.

Jeshi Stars inatarajia kuwa na wakali Monalisa Kaijage, Anamary Cyprian  na Noela Uwendamweno huku Pazi Queens ikiwa na Maria Mbena na Tumpale Mwantembe.

Kwa upande wa Dar City itakayocheza na Srelio iliyoichapa pointi 72-71, itaongozwa  na Sharon Ikedigwe, Amin Mkosa, Ally Abdallah, Clinton Best na Jamal Marbuary, huku Srelio ikiwa na Junior Louissi, Lerry Mve na Badru Bilali.

Pazi katika mchezo wake dhidi ya ABC itakuwa na Soro Geofrey, Josephat Petar na Robert Tasire, na ABC itakuwa Enerco Agustino , Elias Nshishi na Alinani Msongole.

KIKA 02


Robo fainali itaendelea  kesho kutwa (Jumapili) kwa upande wanawake na DB Lioness itacheza dhidi ya Polisi Stars, Tausi Royals na DB Troncatti na upande wa wanaume, JKT itachuana na Savio, huku Stein Warriors ikimalizana na UDSM Outsiders.

Kila timu itacheza mara tatu ‘best of three play off’, na mshindi wa michezo miwili mfululizo itaingia nusu  fainali.  

KIKA 04


KIKA 04

TAUSI ROYALS, POLISI STARS HAZITABIRIKI

Katika michezo hiyo, mchuano mkali unatarajiwa kuwepo kwa timu sita, JKT Stars, Jeshi Stars, DB Lioness, Polisi Stars,  Tausi Royals,  na Vijana ‘City Bulls’.

Polisi Stars na Tausi Royals zimekuwa hazitabiriki katika michezo yao na lolote linaweza kutokea kutokana na ushindani walioonyesha.

KIKA 03


Ikiwa ni mara ya pili Tausi Royals kushiriki ligi hii ya WBDL, imekuwa ikionyesha  ushindani mkubwa kwa timu kongwe, kutokana na kujituma na kutabiriwa itafanya vizuri msimu huu.

Kwa upande wa Polisi Stars ambayo itacheza dhidi ya DB Lioness ilianza kuonekana katika mchezo dhidi ya wapinzania hao hao katika mchezo wa kwanza na waliichapa kwa pointi 58-55.

Tausi Royals na DB Troncatti zitakutana katika mchezo wa pili, huku wa kwanza Tausi ilishinda kwa pointi 78-48.

Licha ya DB Troncatti na Pazi Queens kupata  nafasi ya kucheza robo fainali, hazijazoea mikiki mikiki ya ligi hiyo.

KIKA 01


Baada ya kuonyesha ubora wao katika michezo 15, Jesca Ngisaise wa  JKT Stars na Ntibonela Bukeng kutoka Savio walikuwa kivutio na wanasubiriwa kuona kama kasi yao itakuwa ile ile hatua ya robo fainali.

Moja ya sifa yao ni uwepo wao kila eneo la nafasi kwa wachezaji  wanaofanya vizuri na eneo la ufungaji, Jesca aliongoza kwa kufunga pointi 584, akimwacha kwa mbali Elina Sinasenga  wa Twalipo Queens kwa pointi 231 akifunga 353.

Nafasi ya tatu alichukuliwa na Taudensia Katumbi kutoka DB Lioness aliyefunga pointi 343, huku ya nne ikienda kwa Anamary Cyprian (Jeshi Stars 280) na Jesca Lenga (DB Troncatti 273).

Jesca aliongoza tena kwa kufunga katika eneo moja la mtupo mmoja wa ‘three points’ akifunga 59, akifuatiwa na Irene Gerwin (DB Troncatti) 38, Monalisa Kaijage (Jeshi Stars) 37, Jesca  Lenga (DB Troncatti) 23 Jacqluelyn Masinde (Polisi) 22.

Kwa upande wa utoaji wa asisti, alishika nafasi ya tatu kwa kutoa 74, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Noela Uwendameno (Jeshi Stars) aliyetoa mara 172,  Jesca Lenga (DB Troncatti) akishika nafasi ya  pili kwa kutoa 74.

Upande wa ‘Steal’, Jesca alishika nafasi ya tano, baada ya kunyakua  mpira mara 23, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Noela Uwendameno aliyenyakua mara 32.

Kwa upande wa Bukeng aliongoza kwa kufunga pointi 372, akifuatiwa na Godfrey Swai wa Savio aliyefunga 277.

Upande wa ‘Steal’, alishika nafasi ya pili kwa ni baada ya kunyakua mara 21, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Osward Bera (DB Oratory) aliyenyakuwa mara 25.