Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Mwaluko Kabudi (wa nne kutoka kushoto waliokaa), akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wadau wa sekta ya habari na utangazaji baada ya kufungua Mkutano wa Wadau wa Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki uliofanyika Agosti 21, 2025 jijini Dar es Salaam.
Waliokaa kutoka kulia ni Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Patrick Kipangula, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Mbuya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa, Msemaji na Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Tanzania (DCP) David Misime pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Waliosimama nyuma ni viongozi wa Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) akiwemo Muhidin Issa Michuzi @issa_michuzi (Mdhamini), Mwenyekiti wa TBN Beda Msimbe, Mjumbe Joachim Mushi na Mweka Hazina ambaye pia ni Mtaalamu wa Habari, Cathbert Kajuna @iamkajunason