Beki Mtanzania anukia Kenya | Mwanaspoti

Nyota huyo ambaye ni zao la timu ya vijana ya Dodoma Jiji chini ya miaka 20, ameondoka ndani ya kikosi hicho baada ya mkataba wake kuisha, huku ikidaiwa aliomba kutoongeza mwingine kwa lengo la kutafuta changamoto sehemu nyingine mpya.

“Nafikiria baada ya muda tutakuwa tumekamilisha kila kitu lakini hatuwezi kusema tumefikia wapi kwa sasa kwa sababu ni siri kati ya pande mbili, suala la kucheza Kenya au kwingineko litategemea na makubaliano yetu,” kilisema chanzo hicho.

Awali, uongozi wa Pamba Jiji ulifanya mazungumzo na nyota huyo kwa lengo la kumsajili, ingawa dili hilo lilikwama baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya maslahi binafsi, hivyo kuiacha KCB ikiwa ndio timu pekee inayoiwinda saini yake.

Baada ya Pamba Jiji kushindwa kufikia mahitaji ya nyota huyo, ndipo ikatafuta mbadala wake ambapo ilikamilisha usajili wa beki, Hassan Kibailo aliyejiunga na kikosi hicho, kufuatia mkataba wake na Namungo FC ‘Wauaji wa Kusini’ kumalizika.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata zinaeleza kuwa nyota huyo yupo katika hatua nzuri za kujiunga na KCB, huku menejimenti yake ambayo ndio inayomsimamia ikiwa tayari imeshafanya mawasiliano na kilichobakia ni mambo machache ya kumalizia tu.