Hai. Mtiania wa urais wa Tanzania kwa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu amesema uongozi haupimwi kwa umri bali kwa uwezo wa akili na hofu ya Mungu..
Mwalimu ameyasema hayo aliposimama kusalimia wananchi wa mji wa Bomang’ombe waliojitokeza barabarani kumlaki akiwa njiani kuelekea Moshi kutoka Arusha.
“Msiniangalie kwa umri wangu, nipimeni kwa uwezo wangu na hofu ya Mungu,” amesema na kuongeza;
“Kama uongozi ni umri, tumechagua wazee kwa miaka 60 mambo yamebaki vilevile tu, mwaka huu nichagueni mimi Salum Mwalimu ninawahakikishia sitawaangusha,” amesema

Leo, Mwalimu anatarajia kuhitimisha ziara yake mikoani, tangu alipoanza Jumamosi Agosti 16, 2025 akisaka wadhamini katika safari yake kuusaka urais wa Tanzania.