Na Mwandishi Wetu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)kimempitisha mwanachama wake Dougras Didas MASABURI kuwa Mgombea ubunge wa Jimbo la Kivule jijini Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Masaburi ambaye aliongoza katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama hicho ametangazwa kuwa mgombea ubunge katika Jimbo hilo baada ya Halmashauri Kuu ya CCM kukaa kikao chake jijini Dodoma kwa ajili ya kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wake wa ubunge ambao sasa watapeperusha bendera katika Uchaguzi huo.
Taarifa iliyotolewa na CCM imetaja wagombea katika majimbo yoye nchini na kwa Jimbo la Kivule aliyepitishwa ni Masaburi.
Baada ya kupitishwa kwa jina lake Masaburi kwa mujibu wa utaratibu atachukua fomu ya kugombea ubunge na kisha kuirejesha katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na hatimae kusubiria kampeni kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi katika Jimbo la Kivule.
Kwa kukumbusha tu Jimbo la Kivule ni Jimbo jipya ambalo limepatikana baada ya Tume Huru ya Uchaguzi kuligawa Jimbo la Ukonga na kupatikana majimbo mawili ambayo Ukonga na Kivule na Jimbo hilo la Kivule Mgombea wake ni Masaburi.