Ateba ndio basi Simba, apewa miwili Iraq

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Leonel Ateba sasa ni rasmi hatakuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu ujao, baada ya kutua klabu ya Al – Shorta ya Iraq iliyompa mkataba wa miaka miwili akitokea Simba na anatarajia kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ateba aliyeitukikia Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja na kuifungia mabao 13 msimu uliopita amejiunga na timu hiyo baada ya kuuzwa na Simba ambayo iliachana naye kumpisha aliyekuwa kiungo wa Mamelodi Sundowns, Nao Maema.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kililiambia Mwanaspoti kuwa tayari uongozi wa Simba umekamulisha biashara ya kumuuza Ateba kwenda Al – Shorta ya Iraq.

“Ni kweli tumemuuza mshambuliaji huyo baada ya ofa nyingi mezani tumefikia makubaliano nachezaji huyo ambaye alikywa ni lazima auzwe ili kupusha usajili mpya ambao tayari umekamilika ndani ya Simba;

“Mapema tulishazungumza kuwa kutakuwa na biashara ya kumuuza mshambuliaji huyo dili limekamilika wakati wowote klabu itatoa taarifa juu ya biashara hiyo Ateba ameichagua timu hiyo kutokana na uwakilishi wa michuano ya kimataifa.”

Mtoa taarifa huyo alisema Ateba tayari alishaaga wachezaji wenzake akiwa nchini Cairo ambapo timu hiyo imehamishia kambi ikitokea Misri na mwushoni mwa mwezi huu kikosi hicho kinatarajia kurejea nchini kwa ajili ya kujiandaa na tamasha la Simba Day.

Chanzo hicho kilisema dau walilo muuza mshambuliaji huyo ni zaidi ya Sh 600 milioni hivyo ni faida kwako na wanaamini mshambuliaji huyo atakuwa sehemu ya kivutio cha nyota wengine kutamani kuitumikia Simba.

Timu aliyojiunga nayo Ateba imeanzishwa mwaka 1932 imetwaa ubingwa wa ligi hiyo mara 16, ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mara moja na Ligi ya Iraq mara moja, akiwa Simba Ateba aliifunga mabao 13 katika msimu uliopita wa Ligi Kuu na timu hiyo kufika fainali ya Kombe la Shirikishi Afrika.