Kasi ya ukuaji wa uchumi wa taifa la Tanzania imetajwa kuwa kivutio kwa baadhi ya wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali, ikiwemo ya kifedha kuendelea kuwekeza nchini kutokana na uhakika wa soko pamoja na usalama wa mitaji yao.
Hayo yamesemwa na wawekezaji kutoka nchini ghana ambao wamefanya ziara nchini kuja kuangalia maendeleo ya uwekezaji wa moja ya kampuni yao ya utoaji mikopo kwa njia ya mtandao ya OYA ambapo akizungumza rais wa kampuni ya RNAQ ambayo inamiliki lia kamluni ya oya ulimwenguni richard quaye amesema pa moja na ukuaji wa uchumi vitu vingine vilivyo wavutia ni amani na utulivu uliopo hapa nchini.
Kwa upande wake kobinna Tuyee mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi pamoja na Nicholas Armah mkurugenzi wa kampuni wamewataka watanzania na diaspora waliopo nje kuangalia Tanzania na kuona namna ya kuja kuwekeza hasa kutokana na hali ya uongozi imara pamoja na fursa za masoko na biashara zilipo katika taifa la Tanzania.
Naye Alpha Petter mwakilishi wa kampuni ya OYA Tanzania amesema hadi sasa vijana zaido ya elfu 50 wameshapata mikopo kupitia mtandao huu pia kampuni hiyo ikitoa ajira zaidi ya 500 kwa wananchi na kuwa na mchango katika ukuaji wa taifa la Tanzania