TIB Yashiriki Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji wa Taasisi za Umma Arusha

Benki ya Maendeleo TIB, ikiwa benki ya maendeleo nchini yenye jukumu la kipekee la kuchochea maendeleo ya taifa, ni miongoni mwa taasisi za umma zinazoshiriki kikao kazi Kikao Kazi cha Wakurugenzi wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kinachoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.

Kwa miaka kadhaa, TIB imeendelea kuwa mshirika madhubuti wa Serikali katika kufanikisha uwekezaji wa kimkakati unaolenga kuongeza uwekezaji wa ndani na ajira kupitia miradi ya maendeleo. Uwekezaji huo unahusisha sekta za kilimo cha kibiashara, viwanda, nishati safi, huduma za kijamii kama maji safi, afya, elimu, utalii pamoja na miundombinu.

Vilevile, benki hiyo imeendelea kuwa kinara katika utekelezaji wa sera za Serikali za kukuza uchumi wa viwanda na kuimarisha sekta binafsi kwa kutoa mikopo nafuu ya muda mrefu inayowawezesha wawekezaji wa ndani kushiriki kikamilifu katika uchumi wa taifa.