UDOM YAKUTANA NA WADAU KUCHAMBUA NAFASI YA AKILI UNDE KATIKA UTAWALA BORA

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwa kushirikiana na wadau wa teknolojia na wataalamu wa utawala wamekutana leo Jijini Dodoma chuoni hapo kwenye warsha maalumu inayolenga kuchambua nafasi ya akili unde katika kuimarisha misingi ya utawala bora nchini.

Akizungumza mara baada ya kufungua warsha hiyo leo Agosti 25,2025 Naibu Makamu Mkuu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) – Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Prof. Razack Lokina amesema wananangazia kuhusu matumizi ya akili Hunde na namna ya kuimarisha utawala bora na kuongeza ufanisi katika utendaji wa Serikali

“Suala kubwa ni katika kungalia matumizi bora ya akili hunde namna ambavyo inaweza kusaidia katika sekta ya Afya na kilimo pamoja na kujadili changamoto zake endapo itatumika vibaya ni wapi inaweza kuharibu lakini ikitumika vizuri inaweza kuongeza ufanisi katika utendaji wa Serikali, “amesema.


Amesema suala hilo kwa wao kama wana taaluma ni muhimu kuliongelea kwasababu tayari lipo duniani na hawawezi kulikwepa kwani changamoto mbalimbali wameanza kuzuiona kutokana na baadhi kuitumia vibaya japo inaweza kuwa vizuri katika kuboresha maisha ya binadamu na kizazi kijacho.

“Huu ni wakati mwafaka wa kuweza kulijadili kwa uwazi na kuweza kuchanganua kila eneo ambalo namna gani akili Hunde inaweza ikatumika kwa ubora zaidi kuliko ambao watu wanaweza kuichukua labda wakatimia vibaya.

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi wa Africa Artificial Intelligence Lab (AfriAI Lab), UDOM Dkt. Mohamed Mjahid amesema mradi huo ulianza mwaka 2021, ambapo katika warsha hiyo watajadili namna bora ya uwazi katika mifumo ya Serikali na sekta binafsi.

“Pia kupitia warsha hii tunajidiliana kuhusu matumizi ya akili unde ili kuweza kutoa uaminifu kwa wananchi na wadau wengine kiamini mifumo ya Serikali katika namna nyingine ya matumizi, “amesema.

Sanjari na hilo Dkt. Mjahid amesema akili unde isipotumika vizuri inaweza kuharibu mifumo mbalimbali ikiweno kudharirisha watu vitu ambavyo sio sahihi pamoja na utoaji wa taarifa zisizo sahihi.