Profesa Kitila: Mimi ni mtumiaji mzuri Vodacom na Mwananchi

Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema anaziheshimu na kuzithamini kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa umuhimu wake kijamii na kitaifa. 

Katika kuthibitisha hilo amesema yeye ni ni msomaji mzuri wa habari zinazotolewa na kampuni ya Mwananchi kila uchwao na pia ni mtumiaji wa Vodacom tangu anaanza kutumia simu yake ya kwanza.

Ameyasema hayo leo Jumanne, Agosti 26, 2025 kwenye uzindunzi wa mfumo jumuishi wa Mazingira, Kijamii na Utawala (ESG) wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL). 

“Tangu nimeanza kutumia simu za mkononi muda wote nimetumia wa Vodacom pekee nashiriki na kusoma kila siku makala za Mwananchi na The Citizen,” amesema.

Amesema kampuni hizo kuelekea dira ya Maendeleo ya 2050 ni muhimu kijamii na kiuchumi na ushirikiano wao muhimu unatija katika mchakato wa maendeleo.

“Lazima tuwawezeshe watu wetu ili kuhakikisha kwamba ulimwengu wa kiditijali unakuwa muhimu katika ujumuishi na hata masuala ya kifedha,” amesema.