New York. Gavana wa Benki Kuu ya Marekani, Lisa Cook amemshitaki Rais Donald Trump, baada ya kutangaza kumfuta kazi.
Tangu aingie madarakani muhula wa pili, Rais Trump amekuwa na utaratibu wa kuwafuta kazi watumishi tangu alipoingia madarakani mapema mwaka huu. Alimfukuza kazi Gwynne Wilcox, mwanamke wa kwanza Mweusi kuketi katika Bodi ya Kitaifa ya Mahusiano ya Kazi, ambayo inasikiliza mizozo ya wafanyikazi katika sekta ya kibinafsi.
Lakini pia amewafuta kazi maafisa kadhaa kutoka mashirika mengine ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakichukuliwa kuwa huru kutoka kwa Ikulu ya White, hali ambayo imeonekana si sawa na kupingwa na baadhi ya viongozi ikiwemo Lisa Cook.
Aliyeng’olewa katika nafasi yake ya Ugavana wa benki kuu ya Marekani, Agosti 25 mwaka huu kwa tuhuma za ulaghai wa mikopo ya nyumba mwaka 2021.
Katika kesi hiyo Cook amesema, Trump hana uwezo wa kumwondoa madarakani, na amekiuka haki yake ya kufuata utaratibu chini ya Katiba ya Marekani kwa kumfukuza kazi bila kuanzisha vita vya kisheria ambavyo vinaweza kupinga kanuni zilizowekwa kwa muda mrefu.
Amesema Trump pia amekiuka sheria ya nchini iliyomruhusu kumwondoa gavana wa Benki Kuu na amechukua hatua ambayo haijawahi kufanywa na Rais yeyote wa taifa hilo.
“Si aina ya kosa ambalo Rais alitaja wala ushahidi usio wazi dhidi ya Gavana ungekuwa sababu ya kuondolewa hata kama madai ya Rais yalikuwa ya kweli ambayo sivyo,” amesema Cook.
Ameongeza kuwa Rais hana sababu ya kumwondoa Gavana hata kama alikuwa na ushahidi kwani ni kinyume na utaratibu chini ya Katiba ya Marekani inayozuia kumfukuza mtu kazi bila taarifa au kusikilizwa.
Kwa upande mwingine benki kuu imeeleza kuwa itatii uamuzi wowote wa mahakama na Rais Trump ikiwa mamlaka iliyotumika kutoa uamuzi ni halali.
Hata hivyo wataalamu wengi wameshauri kufanyika kwa uchunguzi wa shughuli zilizotangulia kuteuliwa kwa kiongozi huyo kama zilikuwa kwenye rekodi ya umma kwani fomu rasmi ya ufichuzi wa kifedha ya 2024 kuhusu kiongozi huyo zinaorodhesha mali zinazoshikiliwa na Cook ambazo alizipata kwa ulaghai huo, ikiwemo makazi binafsi.
Wamesema ufichuzi huo pia umeonyesha kuwa viwango alivyotumia kulipa makazi yake ya kibinafsi vilikuwa vya juu kuliko wastani wa kitaifa wakati huo.
Elidaima Mangela (UDOM) kwa msaada wa Mashirika ya habari