DK.ASHA-ROSE MIGIRO AAHIDI CCM KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU UCHAGUZI MKUU

Na Mwandishi Wetu,Ngerengere

KATIBU Mkuu wa Chama Cua Mapinduzi(CCM) Balozi Dk.Asha -Rose Migiro amewahakikishia Watanzania kuwa Chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinafanya kampeni za kistaarabu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Balozi Dk.Migiro amesema hayo Agosti 29,2025 katika Uwanja wa Njia Nne uliopo Kata ya Ngerengere mkoani Morogoro wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea Urais wa CCM ,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea na ziara yake kuomba kura kwa watanzania ili wamchague katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

“Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na

Mgombea Urais wetu ulitupa maelekezo CCM iwe mfano wa uendeshaji bora na kistaarabu katika kampeni na uchaguzi Mkuu mwaka huu.Napenda kuhakikisha maaskari  wote wa CCM tumejipanga kufanya kampeni za kistaarabu.”

Aidha amesema kuwa maelfu ya wananchi wanaojitokeza katika mikutano ya kampeni za mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan ni ishara ambavyo viongozi wamejipanga na kubwa zaidi Oktoba wananchi TUNATIKI.