Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akihutubia maelfu ya Wananchi na Wanachama wa Chama hicho ambao walijitokeza kwenye Viwanja vya Furahisha Vilivyopo Jijini Mwanza.
Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi yupo kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya Kufanya Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi akiwa ni mgombea mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametumia Fursa hiyo kunadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025-2030 pamoja na kuwanadi Wagombea wa Chama hicho katika nafasi ya Ubunge na Udiwani ndani ya mkoa huo.