MZEE JOSEPH BUTIKU ALIVYOIBUKIA KATIKA MKUTANO WA KAMPENI WA DK.EMMANUEL NCHIMBI RORYA

MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi amekutana na kusaliamiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Joseph Butiku wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu .

Dk.Nchimbi ambaye alikuwa akiendelea na kampeni katika Mkoa wa Mara, alifanya mkutano katika Uwanja wa Ubwere Jimbo la Rorya,ambako alipokelewa na Butiku aliyekuwa moja ya viongozi waliokuwepo eneo la mkutano ambapo walisalimiana na kuteta kidogo kabla ya Dk.Nchimbi kuzungumza na maelfu ya wananchi waliofika kumsikiliza.

 

Akihutubia wananchi wa Rorya mkoani Mara katika muendelezo wa mikutano ya kampeni Balozi Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Rorya, Jafari Chege sambamba na Wagombea Ubunge wengine pamoja na Madiwani wa Mkoa huo.

Dkt. Nchimbi anaendelea na kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania  kuwaongoza katika awamu nyingine ya miaka mitano, katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.