Ulisikia kocha wa Simba, Fadlu Davids akidai kwamba kikosi chake kinakosa mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kuamua mechi akitumia neno X- factor? Basi Yanga imemjibu.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amemjibu Fadlu kiaina akisema timu yao wala haina shida na wachezaji wenye ubora huo.
Kamwe amesema Yanga ina wachezaji wengi wenye ubora wa kuamua mechi ambao wengine wameshawaongezea X wakiwa nazo tatu.
“Nimesikia kuna watu wanalia hawana wachezaji X- factor, nyie waandishi mmejaribu kuelezea lakini wengi wenu hamjaelewa vizuri,” amesema Kamwe na kuongeza:
“Unapoambiwa mchezaji mwenye sifa za X – Factor ni yule mwenye uwezo mkubwa wa kuamua mechi, sasa hebu tuangalie kwenye ti yetu ya Yanga. Tuanze na Maxi Nzengeli yule anaweza kuamua mechi, Clement Mzize naye anaweza kuamua mechi. Twende kwa Pacome (Zouzoua) naye ndio usiseme.
“Tena huyu Pacome msimu uliopita ndio alikuwa na X – Factor, lakini kuanzia msimu ujao atakuwa na hizo X – Factor tatu kutokana na daraja lake la ubora alilokuwa nalo.”