Serikali imetoa wito kwa klabu kongwe za Simba SC na Yanga SC, ambazo kwa sasa hutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, kuhakikisha zinakuwa na viwanja mbadala vya kuchezea michezo yao endapo zitaarifiwa kuacha kutumia uwanja huo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo matukio ya kitaifa au matengenezo.
Akizungumza, msemaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema hatua hiyo inalenga kuepusha migogoro, malalamiko na mvutano unaojitokeza mara kwa mara pale klabu hizo zinapokumbana na changamoto ya kutopata uwanja huo kwa muda fulani.
Aidha, imeelezwa kuwa serikali itabaki mmiliki na msimamizi mkuu wa uwanja huo wa taifa, hivyo ni wajibu wa vilabu husika kuwa na maandalizi ya mapema ili kuendelea na ratiba zao bila vikwazo.
Related