OFISI ZA JAMII FORUMS ZADAIWA KUVAMIWA


 ::::::

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo, amesema Ofisi zao zimevamiwa na kwa kile alichodai kuwa uvamizi ulikuwa na Lengo la kumtafuta yeye

Kupitia ukurasa wa Melo amechapisha taarifa inayosomeka “Kuna ‘uvamizi’ usio rafiki uliofanyika muda sio mrefu katika ofisi za JamiiForums, Mikocheni jijini Dar wakinitafuta mimi .. Nalaani vitendo kama hivi, ila umma utaujua ukweli hivi karibuni”

Torch Media tunaendelea kufanya jitihada za kuwautafuta uongozi wa Jamii forums na Jeshi la Polisi kufahamu kwa kina juu ya taarifa hizo