Dar es Salaam, 4 Septemba 2025 – Kampuni ya michezo ya
kubashiri PigaBet leo imetangaza kwa shangwe majina ya washindi wa promosheni
zake kubwa mbili – SHINDA NDINGA na JISMATISHE, katika droo iliyofanyika jijini
Dar es Salaam.
Mshindi wa promosheni ya SHINDA NDINGA ni Musa Nicodemus
kutoka mkoa wa Mwanza, ambaye ameibuka na zawadi ya smartphone ya kisasa kupitia
kampeni hiyo ya kipekee.
Washindi wa JISMATISHE
Hamis Kassim kutoka Tegeta, Dar es Salaam – amejinyakulia
Smart TV aina ya Hisense yenye ukubwa wa inch 55.
Innocent Sanga kutoka Arusha – ameibuka mshindi wa
smartphone ya kisasa aina ya Samsung.
Akizungumza baada ya kutangazwa kwa washindi, Meneja
Mawasiliano wa PigaBet, Hemed Jaafary Msonge, alisema:
“Tunafurahi kuona wateja wetu wakiendelea kufurahia
promosheni zetu na kushinda zawadi kubwa. Hii ni njia yetu ya kurudisha
shukrani kwa wachezaji wote wanaotuamini kila siku.”