Bunge la Thailand limemchagua mfanyabiashara Anutin Charnvirakul kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, ikiwa ni kiongozi wa tatu kushika nafasi hiyo katika kipindi cha miaka miwili.
Anutin, ambaye ni kiongozi wa chama cha Bhumjaithai, alipata uungwaji mkono wa kutosha bungeni baada ya chama chake kujitenga na muungano wa Pheu Thai uliokuwa ukiongozwa na Paetongtarn Shinawatra.
Wiki iliyopita, Mahakama ya Kikatiba ilimuondoa Paetongtarn madarakani kwa tuhuma za ukiukaji wa maadili katika namna alivyoshughulikia mzozo wa mpaka kati ya Thailand na Cambodia.
Wachambuzi wanasema kuteuliwa kwa Anutin ni pigo kubwa kwa familia ya Shinawatra, ambayo imekuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Thailand tangu mwaka 2001, alipokuwa Waziri Mkuu Thaksin Shinawatra, baba wa Paetongtarn.
Hata hivyo, wachambuzi pia wanatahadharisha kuwa huenda changamoto za kisiasa zikaendelea, kwani taifa hilo limezoea migogoro ya mara kwa mara ikiwemo kuondolewa kwa viongozi kupitia maamuzi ya mahakama na mapinduzi ya kijeshi.
Related