::::::::
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, @jamiiforums Maxence Melo, ameomba Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya kujiuzulu ujumbe wa Bodi katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijami wa Instagram wa Melo @macdemelo amechapisha taarifa inayosomeka “Leo, Septemba 06, 2025 nimemuandikia rasmi Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari juu ya uamuzi wangu kujiuzulu ujumbe wa Bodi katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Niliteuliwa Disemba 18, 2023 na nimehudumu kikamilifu majukumu yangu. Natoa shukrani nyingi kwa Wizara, Tume, na wajumbe wenzangu kwa ushirikiano mzuri walionipa katika kipindi chote.
Aidha, naishukuru Taasisi yangu na Bodi ya Wakurugenzi kwa kulipa gharama zote za ushiriki wangu katika vikao vyote na shughuli za Tume kwa takribani miaka miwili.”