Kwa Mkapa ni  nyekundu, nyeupe 

IKIWA saa zinazidi kukatika kabla ya kuanza rasmi shughuli ya utambulisho wa nyota wapya wa kikosi cha Simba kwa msimu wa 2025-2026, ikishindikizwa na mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo na Gor Mahia ya Kenya Kwa mMkapa kunakofanyika tamasha la Simba Day ni nyekundu na nyeupe.

Rangi hizo zinazotumiwa na klabu ya Simba ndio zilizoanikiza uwanja wa Mkapa mbali na zile jezi za rangi bluu.

Mbali ya mashabiki hao, askari wakiwa na farasi pamoja na wale wenye wameendelea  kuimarisha ulinzi kuhakikisha utaratibu unafuatwa nje ya uwanja.

Mashabiki ambao kwa asilimia kubwa wamevalia jezi nyekundu na bluu wameonekana uwanjani hapa wakiwa wanaingia bila ya msongamano wowote licha ya wingi wao.

Mchezo wa Simba dhidi ya Gor Mahia unatarajiwa kuanza saa 1:30 usiku lakini kabla ya mechi hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo shoo kutoka kwa msanii wa Bongo Fleva ‘Mbosso’ ambaye anatamba na vigogo vyake vipya ikiwemo PAWA.