Burudani zatawala nje kwa Mkapa

ACHANA na burudani inayotarajiwa kutolewa baadaye na Simba, lakini hivi sasa nje kuna vaibu lingine linaloendelea kwenye maeneo tofauti karibu na Uwanja wa Mkapa.

Leo ni kilele cha wiki ya Simba Day ambayo hutambulisha wachezaji wapya na benchi la ufundi ikitaambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na mechi ya kirafiki.

Kuna kikundi cha mashabiki mbalimbali ambao wameonekana kwenye matenti wakivalia jezi za Simba.

Kuna wale ambao wanauza bidhaa mbalimbali za vinywaji wameweka miziki na kuwakusanya mashabiki ambao wameonekana wakifurahia nyimbo ya Mnyama ya AliKiba.

Mbali na hao wapo pia wapiga ngoma ambao wameambatana na mashabiki wenzao wakitoa burudani na wengine wakitunzwa fedha na wale wanaoelekea ndani ya uwanja.