Kwa Mkapa kunanoga | Mwanaspoti

TAMASHA la Simba Day linaendelea kupamba moto Benjamin Mkapa ambako idadi kubwa ya mashabiki tayari imeshaingia kiwanjani huku kukiwa na sehemu chache za majukwaa ambazo watu hawajakaa bado.

Licha ya sehemu hizo chache za majukwaa ambazo hazina  mashabiki, nje kuna idadi kubwa ya mashabiki ambao wanaendelea kuingia.

Idadi kubwa ya mashabiki waliopo ndani imeonekana kuwa na vaibu la kutosha ikiwa inashangilia matukio mbalimbali yanayoendelea.

Jukwaa la mzunguko ndio linaonekana kuwa na nyomi ya kutosha na mapengo machache yakiwa upande wa jukwaa la VIP B.

Kwa sasa kuna burudani ya DJ Sinyorita ambaye anatumbuiza baada  ya mchezo wa Simba Veteran dhidi ya JKT Veteran kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.