Dakika 10 za Joh Makini Simba Day

Msanii wa Hip Hop, John Simon Mseke maarufu Joh Makini amepiga shoo iliyoamsha shangwe kubwa kwaa mashabiki ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa akitumia takriban dakika 10.

Joh Makini anayetambulika pia kwa jina la Mwamba wa Kaskazini, amepiga shoo hiyo katika Tamasha la Simba Day linalofanyika leo Septemba 10, 2025.

Shoo ya Joh Makini ilianza saa 10:16 jioni hadi saa 10:26 jioni ambapo aliimba nyimbo tatu kutoka kundi lao la Weusi.

Mwamba wa Kaskazini aliingia na Wimbo wa Wapoloo ambao ulipokewa vizuri na mashabiki waliojitokeza kwa wingi uwanjani huku wakiimba naye pamoja.

Baada ya hapo, ikafuatia ngoma ya Humu Tu ambayo pia iliteka hisia za mashabiki wengi, kisha akamalizia na Gere.

Muda wote wakati Joh Makini akitumbuiza, kulikuwa na mzuka majukwaani kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakiburudika na mziki mzuri.