MSIMU Wa pili Wa Tamthilia ya “NICE TO MEET YOU ” wazinduliwa rasmi Wasanii chipukizi wajipanga kuliteka soko la Filamu nje na ndani kutokana na ubunifu wao kwenye gemu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Lulu Abas maarufu Kama “Lulu diva” amesema Msimu wa Kwanza alifanya vizuri na Kupelekea kupata Tuzo hivyo msimu huo mpya anategemea kupata zaidi tuzo za ndani na nje kutokana na uhusika wake kuboreshwa zaidi.
“Msimu wa Kwanza nilifanya vizuri lakini kutokana na kupata kwangu tuzo kumenizidishia morali hivyo msimu wa pili Watson vingi vizuri zaidi wakae tu karibu na televisheni zao.”
Aidha Nae Hemed PhD ameongeza kuwa Watazamaji walipie Visimbuzi vyao ili kuendelea kuona tamthilia hiyo ambayo kuna vichwa vingi damu changa ns wakongwe ambao wanajua nini soko linahitaji kwa wakati huu.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema Startimes ina dhamira ya dhati kuhakikisha filamu za Kitanzania zinapewa Kipaumbele na huo ndio mwanzo tu hivyo watazamaji wa kisimbuzi hicho wategemee mazuri zaidi hasa Mwezi huu wa Septemba katika kunogesha Kampeni yetu ya “ZOTE NDANI”.
“Msimu huu wa pili wa tamthilia iliyobeba uhusika wa Wasanii kutoka kiwanda cha Filamu nchini zikiwemo damu changa tumeona tuendelee kuwapa sapoti lengo ni kuwaonesha Watanzania kuwa sisi Kama Startimes tumejipanga kuwapa Maudhui mbalimbali na Kuinyanyua sekta hii ya Filamu nchini”.
Aidha Malisa pia amesema tamthilia hiyo itakuwa ikiruka kila Jumatatu hadi Ijumaa Kupitia St Swahili kuanzia saa 3 Usiku Katika Kifurushi cha chini kabisa lengo ni kuwapa burudani watu wote.