MENEJA TRA TEMEKE AONGOZA ELIMU YA KODI MLANGO KWA MLANGO TEMEKA NA KIGAMBONI

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza zoezi la elimu ya kodi mlango kwa mlango kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke mkoani Dar es salaam kwa lengo la kutoa elimu, kusikiliza changamoto na kuwakumbusha wafanyabiashara kufanya malipo ya awamu ya tatu kwa wakati. 

Zoezi hilo lililoanza Jumatatu wiki hii, limezinduliwa rasmi jana tarehe 09.09.2025 na Meneja wa TRA mkoa wa Kikodi Temeke,  Masau Malima ambae pia alishiriki kutoa elimu ya kodi na kuwasikiliza wafanyabiashara wa Keko wilaya ya Temeke. 

Akizungumzia zoezi hilo,  Malima amsema lengo la zoezi hilo ni kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya mambo mbalimbali ya kodi, kusikiliza changamoto zao, kuchukua maoni yao kwa lengo la kuboresha huduma za TRA na kuwakumbusha kulipa kodi  awamu  ya tatu kabla au mnamo tarehe 30.09.2025 ili kuiwezesha serikali kukamilisha miradi ya maendeleo na kijamii kwa wakati.

” Lengo la zoezi hili ni kupita kuonana na wateja wetu kuwapatia elimu na kuchukua changamoto zao na kuzitatua” 

Aidha, ametoa wito kwa wafanyabiashara kufanya malipo ya awamu ya tatu pamoja na kodi nyingine na kuwakaribisha kutembelea ofisi za TRA ili kuwahudumia na kuwasikiliza changamoto zao kwa lengo la kuzitatu. 

Kwa upande wake mmoja wa wafanyabiashara wa Keko,  Bakari ameeleza kuwa ujio wa Meneja katika eneo la biashara umeonyesha njia na kuwahamasisha wao kulipa kodi kwa hiari  na kuwa wapo tayari kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa kwani mataifa yote yaliyoendelea duniani ni kutokana na kodi wanazolipa wananchi. 

” Kwa utaratibu huu hata sisi mafundi, wafanyabiasha kulipa kodi bila ya shida kwa sababu Meneja tayari ameonesha njia kuwa kuna urafiki kati ya wafanyabiashara na TRA ” 

Nae, . Bilina Johnson ametoa rai kwa wafanyabiashara wengine kuwa wanapotembelewa na watu wanaojitambulisha kama  watumishi wa TRA kuhakikisha wanajiridhisha kwa kukugua vitambulisho vyao ili kuepuka matapeli wanaojitambulisha kama maafisa wa TRA.