Lulu Diva Afunguka Kuhusu Tuhuma za Kutoka na Ex wa Mobetto – Global Publishers



Staa wa muziki na filamu Bongo, Lulu Diva @luludivatz amefungukia tuhuma za kutoka kimapenzi na aliyekuwa X wa Hamisa Mobetto, Kelvin Sowax kabla hajaolewa.

Lulu Diva amesema ni kweli alikuwa na uhusiano na mwanaume huyo lakini wakati wanaanza, alikuwa tayari ameshaachana na Hamisa Mobetto na kueleza kwamba hakuna tatizo kutoka na mtu aliyewahi kuwa na uhusiano na mtu mwingine kisha wakaachana.