USALAMA umezingatiwa katika hitimisho la Wiki ya Mwananchi, huku askari wakionekana katika maeneo yote ya nje ya uwanja wa Benjamin Mkapa na biashara zikiendelea mdogomdogo.
Hii yote ni kuhakikisha kwamba usalama wa mashabiki na mali zao unazingatiwa. Lakini, si hivyo tu yapo maeneo ambayo yamezungushiwa kamba za rangi nyekundu na nyeupe kama uzio ambayo ni mahali pa watu kupita.
Vilevile wapo Askari waliosimama katika maeneo tofauti na wengine wakiwa wanazunguka na farasi, huku wote wakiwa na silaha za moto mikononi.
Kwa upande wa mashabiki wanaendelea kuingia na hali ikiwa shwari wakionekana kufuata utaratibu uliowekwa.
Nje ya uwanja biashara ya kuuza jezi, vyakula na vinywaji inaendelea taratibu mashabiki wengi wakionekana kuingia ndani na kuacha maeneo hayo kuwa wazi.