Ngome Yazidi Kung’ara BAMMATA – Global Publishers



Timu za Ngome zinazomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania zimezidi kung’ara katika mashindano ya  Michezo mbalimbali ya Majeshi (BAMMATA) ambayo yanafanyika mjini  Zanzibar.

Baadhi ya michezo ambayo inaongoza  hadi sasa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa mikono (handball), mpira wa pete pamoja na riadha.

Katika michezo iliyofanyika jana tarehe 11 Agosti 25, kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu timu ya Ngome ilifanikiwa kuifunga timu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) goli 1-0  mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa Mao Tse Tung.

Mchezo mwingine ulikuwa ni mpira wa kikapu uliozikutanisha timu za Ngome na JKT ambapo Ngome iliibuka kidedea kwa kuichapa  JKT  alama  81 dhidi ya 57.

Kwa upande wa mchezo wa wavu uliozikutanisha timu za Ngome na Polisi katika uwanja wa Amani, Ngome  ilishinda  jumla ya seti 3-0 na kuzidi kujiweka nafasi ya kufanya vizuri.

Kwa upande wa mchezo wa riadha, timu ya  Ngome imeendelea kuongoza Mita 100 fainali  ya wanawake na kufuzu medali ya dhahabu huku timu ya riadha Ngome Wanawake Mita 5000 ikishika nafasi ya kwanza,  na pia timu ya riadha Ngome wanaume na Wanawake Mita 10,000 .

Matokeo haya yanaipa timu ya Ngome kuwa na uwezekano mkubwa wa  kutwaa  ubingwa wa mshindi wa jumla.