Dogo Paten aibua shangwe kwa Mkapa

Msanii wa Singeli maarufu kama Dogo Paten ameibua shangwe kwa mashabiki baada ya kupata nafasi ya kutumbuiza saa chache baada ya mchezo wa kwanza wa ufunguzi ambapo Yanga Orincess imecheza na Mashujaa Queens.

Wimbo Paten wa Afande umeibua hisia kubwa na kupokewa kwa swangwe na mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwa Mkwapa katika tamasha la Wiki ya Mwananchi.

Msanii huyo ambaye amejizolea umaarufu kupitia wimbo huo ameimba sambamba na mashabiki ambao wameonyesha kuvutiwa na wimbo huo.

Baadhi ya mashabiki wamesimama kumpa nguvu msanii huyo ambaye anazunguka kwenye majukwaa kuimba sambamba nao.

Mbali na wimbo wa Afande, msanii huyo amewagandisha mashabiki kwa Mkapa baada ya kuimba wimbo wake wa Singeli mchano ambao pia uliibua shangwe na kuufanya uwanja mzima kuzizima kwa mashabiki kuitikia kwa kuimba.