Washindi Wajinyakulia Televisheni, Simu na Zawadi Nyingine Katika Minada ya PIKU Afrika

Matukio mbalimbali washidni wakikabidhiwa zawadi zao leo Septemba 13, 2025 jijini Dar Esalaam.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa PIKU Afrika, Barnabas Mbunda kulia waliokaa akizungumza wakati wa kuwakabidhi zawadi washindi wa awamu ya tatu jijini Dar es Salaam leo Septemba 13, 2025.

JUKWAA la kidijitali la PIKU Afrika, linalojihusisha na uendeshaji wa minada ya kipekee kupitia mtandao, leo Septemba 13, 2025 limetangaza na kukabidhi zawadi kwa washindi wa awamu ya tatu ya promosheni yake ya minada ya kidijitali.

Katika hafla hiyo, washindi watatu bora waliibuka na zawadi mbalimbali kama ifuatavyo, mshindi wa Kwanza, Jakson Ngonji, alijinyakulia Televisheni janja ya inchi 55 kutoka kampuni ya LG pamoja na ruta yenye kifurushi cha intaneti cha mwaka mzima.

Mshindi wa Pili, Jonathan Paul, alipata kombo ya bidhaa za kiume ikiwemo pafyumu, vidani vya mkononi, na saa ya kisasa.

Mshindi wa Tatu, Niovita Shayo, alijishindia simu janja aina ya Samsung pamoja na spika ya Bluetooth.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa PIKU Afrika, Barnabas Mbunda, amesema kuwa ni mafanikio makubwa kuona zaidi ya washindi tisa wamejinyakulia zawadi mbalimbali kwa kushiriki mnada kwa njia ya kidijitali.

“Hii kwetu PIKU Afrika ni fahari sana. Washindi wamepata zawadi zao bila kikwazo, hali inayodhihirisha uwazi na ubunifu wa mfumo wetu,” amesema Mbunda.

Amebainisha kuwa zawadi mbalimbali zilitolewa, ikiwa ni pamoja na “makombo” ya bidhaa kwa bei ya chini na ya kipekee. Pia ameeleza kuwa bidhaa zote za kielektroniki ambazo washindi wamepata tayari zimekatiwa bima ya mwaka mzima, hivyo washiriki hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu usalama au uimara wa bidhaa hizo.

Mbunda aliongeza kuwa promosheni inaendelea, na minada mikubwa zaidi bado iko mbele. Alieleza kuwa zawadi kuu kwa sasa ni:

Gari aina ya Toyota Raum ikiwa ni zawadi ya funga mwaka. Gari hiyo itatolewa pamoja na Mafuta lita 100 kila mwezi kwa mwaka mzima,Matengenezo ya bure kwa mwaka, Bima kamili ya mwaka mzima.

Pikipiki mpya aina ya TVS, itakayokabidhiwa ikiwa na helmeti na reflector,Kadi ya mafuta lita 30 kwa kila mwezi kwa mwaka mzima,bima ya mwaka mzima.

Namna ya Kushiriki na Tiketi za MnadaKwa wale wanaotaka kushiriki, PIKU Afrika imeweka utaratibu rahisi wa ununuzi wa tiketi kama ifuatavyo:

Tiketi 10 kwa Sh. 1,000

Tiketi 50 kwa Sh. 5,000

Tiketi 100 kwa Sh. 10,000

Tiketi 1,000 kwa Sh. 100,000

Mbunda alisisitiza kuwa kadri idadi ya tiketi inavyoongezeka, ndivyo nafasi ya kushinda inavyokuwa kubwa zaidi.

Kwa upande wake, Jakson Ngonji, mshindi wa kwanza wa Televisheni janja ya inchi 55, ameeleza kwa furaha namna alivyoshinda zawadi hiyo kubwa kwa kutumia dau dogo kupitia mfumo wa mnada wa kidijitali wa PIKU Afrika.

“Nilishiriki kwa matumaini na kwa kweli siamini hadi leo. Nawahamasisha vijana na Watanzania kwa ujumla wajitokeze kushiriki katika minada hii. Ni fursa ya kipekee kupata bidhaa za thamani kubwa kwa gharama ndogo,” amesema Ngonji.

PIKU Afrika inaendelea kuwa kinara katika mapinduzi ya minada ya mtandaoni, ikiwapa Watanzania fursa ya kupata bidhaa bora kwa bei nafuu kupitia mfumo wa kidijitali, wa uwazi, na wa kipekee.