DK.SAMIA:HUWEZI KUSIKIA MTU CCM AKISEMA ‘TUKIWASHE’ LABDA KIWE KING’AMUZI CHA AZAM

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Kasulu

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Chama kinachojali ustawi wa taifa letu la Tanzania usikii mtu kwenye Chama hicho akisema tukiwashe na kama wakisema tukiwashe labda kile king’amuzi cha Azam lakini siyo tukiwashe kwa fujo. 

Dk.Samia ameyasema hayo leo Septemba 13,2025 alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambako ameendelea na mikutano ya kampeni ya kuomba kura kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

“Chama kinachojali ustawi wa taifa letu la Tanzania usikii mtu kwenye Chama hicho akisema tukiwashe na kama wakisema tukiwashe labda kile king’amuzi cha Azam lakini siyo tukiwashe kwa fujo.Kukiwasha kwa fujo hapana.”

Wakati huo huo Dk.Samia Suluhu Hassan ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wana Kasulu na wana Kigoma kuwa kuna msemo unaosema mnyongeni mnyongeni haki yake mpeni.

“Sasa mimi ni mnyonge lakini hivyo niwaombe wananchi wa Kasulu msininyonge.Nipeni tu haki yangu lakini msininyonge.Kwanini msininyonge kwa sababu mimi nafanya kazi ya kuinua Watanzania. Nafanyakazi kuinua ustawi wa maisha ya Mtanzania.

“Nisingependa sana kuwaita wanyonge lakini ningesema watanzania waliopo katika kiwango cha chini tuwanyanyue waje juu.Kwahiyo niwaombe sana ikifika tarehe 29 mwezi wa 10 mwaka huu tuamke mapema.

“Kama tulivyojaza uwanja huu twende tukajaze vituo vya kupiga kura, twende tukakichague Chama Cha Mapinduzi, Chama kazi na Chama kinachojali utu wa mtu.”

Amesisitiza Chama kinachojali ustawi wa taifa letu la Tanzania usikii mtu kwenye Chama Cha Mapinduzi akisema tukiwashe na wakisema tukiwashe labda kile king’amuzi cha Azam lakini siyo tukiwashe kwa fujo. kukiwasha kwa fujo hapana.