DK.SAMIA KUING’ARISHA BUHIGWE KWA UMEME WA UHAKIKA, KUIONGEZEA THAMANI TANGAWIZI

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Kigoma

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk Samia Suluhu Hassan amesema ni ya Serikali ni kuifanya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ing’are kwa umeme na uwe wa kutosha ili kuifanya Buhigwe iwe na uwekezaji wa viwanda.

Akizungumza na maelfu ya wananchi wa Buhigwe akiwa katika muendelezo wa mikutano ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29,Dk.Samia ameeleza mipango ya Serikali katika kuiendeleza Buhigwe.

“Nia yetu ni kuifanya Buhigwe iwe na umeme wa kutosha ili tuweke uwekezaji wa viwanda Buhigwe.Nimeambiwa vijana ni wakulima wazuri wa tangawizi hivyo tunataka tangawizi ile iongezwe thamani.

“Tuweke kiwanda cha kuongeza thamani tangawizi hapa Buhigwe,kwa maana hiyo tunahitaji umeme wa kutosha sio kwa ajili ya tangawizi peke yake lakini pia viwanda vya mazao mengine.

“Kwa maana hiyo tutazalisha umeme pale Maragasi karibia megawati 46 ili kuwa na umeme wa kutosha na kufanya sasa Buhigwe ipate umeme wa kutosha kutoka ule umeme unaozalishwa Maragasi,”amesema Dk.Samia.

Wakati akianza kuzungumza na wanannchi hao ,Dk.Samia Suluhu Hassan ameelezea pia mpango wa Serikali kuhusu na kuanza kwa majaribio ya bima ya afya kwa wote kuanza kwa majaribio kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za huduma za matibabu.

“Tuliahidi kuanza kutekeleza bima ya afya ambayo  tutaanza kwa majaribio halafu tukiona tumeweza tutaifungua kwa nchi nzima ili kila mmoja wetu awe na bima ya afya ajitibie kwa bima yake ya afya.

“Lakini tulisema kwa wale ambao hawana uwezo Serikali itabeba mzigo huo itawatibu kama wananchi wa Tanzania wafaidike na huduma za afya.”

Pamoja na hayo mgombea Urais Dk.Samia ametoa rai kwa wananchi ikifika Oktoba 29 mwaka huu waamke mapema kwa wingi ili kwenda vituo vya kupiga kura kuchagua viongozo.

“Kama tulivyoamka hapa na kuja kwa wingi huu basi hivyo hivyo Oktoba 29  twende vituo vya kupiga kura ili tukapige kura zetu tukachague mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , tukachague mbunge na madiwani.