MAELFU WAJITOKEZA UZINDUZI KAMPENI JIMBO LA ITWANGI


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi.
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Itwangi mkoani Shinyanga

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi, kulia ni Mgeni rasmi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) Munde Tambwe

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Maelfu ya wananchi wa Jimbo jipya la Itwangi Mkoani Shinyanga wamejitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, wakionyesha mahaba makubwa na imani kwa Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Azza Hillal Hamad, wakiahidi kumpa kura za ushindi ifikapo Oktoba 29,2025.

Uzinduzi huo uliofanyika kwa shamrashamra, Jumamosi Septemba 13, 2025 katika Mji wa Didia umehudhuriwa na wananchi, wanachama wa CCM, wagombea udiwani pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM, huku Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) Munde Tambwe Abdallah akiwa mgeni rasmi.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Munde amewaambia wananchi wa Itwangi kuwa wamepata “Mbunge Jembe” mwenye uwezo mkubwa wa kuwatumikia na kuwaletea maendeleo, akisisitiza kuwa anamfahamu Azza tangu akiwa Mbunge wa Viti Maalum kutokana na ujasiri na uwezo wake wa kuwasemea wananchi.

“Azza ni chaguo sahihi. Ni jasiri, mjenga hoja na mtetezi wa wananchi. Nawaomba Oktoba 29 mpigie kura Rais Dk. Samia, Azza Hillal na madiwani wote wa CCM ili tuendelee kupata maendeleo,” amesema Munde.

Akihutubia maelfu ya wananchi, Mhe. Azza Hillal Hamad almewaahidi maendeleo makubwa endapo atapewa ridhaa ya kuongoza Itwangi, akitaja miradi ya maji, afya, elimu na umwagiliaji kuwa kipaumbele chake.

Amesema jimbo hilo linategemea zaidi kilimo cha mpunga na kwamba atahakikisha skimu za umwagiliaji ikiwamo Nyida na nyingine ambazo hazijakamilika zinakamilishwa. Pia ameahidi kusimamia miradi ya maji ikiwemo ule mkubwa wa Ziwa Victoria na ule wa Tinde Package ili kuhakikisha vijiji vyote vinapata huduma.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi.

“Wananchi wa Itwangi, Oktoba 29 nikopesheni imani niwatumikie. Hakuna chama kingine kinachoweza kuwaletea maendeleo zaidi ya CCM,” amesema Azza.

Azza pia amemtaja Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama kiongozi mwenye dira, akieleza jinsi alivyopeleka miradi mikubwa ya kimkakati Itwangi, ikiwamo Reli ya Kisasa (SGR), miundombinu ya barabara, elimu, afya na skimu za umwagiliaji.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo, amemuelezea Azza kama mchapakazi mwenye uchu wa maendeleo, huku Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akisisitiza kuwa chama kina imani kubwa naye kutokana na historia ya utendaji wake.

Aidha, Mbunge Mteule wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Christina Mzamva, amewaomba wananchi kumpa kura Azza, Rais Dk. Samia na wagombea udiwani wote wa CCM.
Ahadi za Azza kwa Wananchi.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM Taifa, Edwin Peter Nyakanyenge wamemuelezea Azza kama kiongozi wanayemuamini kutokana na historia yake ya kutetea maslahi ya wananchi tangu akiwa Mbunge wa Viti Maalum.

Simon Makoye Mayengo

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Simon Makoye Mayengo amesema wananchi wa Jimbo la Itwangi wanapaswa kuendeleza imani yao kwa CCM, kwani chama kimeleta wagombea wanaouzika, makini na wabobevu.

“Kama Mlezi wa Jimbo la Itwangi, tunamshukuru sana Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kutuletea mgombea wetu makini ambaye ni mbobevu katika nafasi hii,alipumzika kidogo na sasa anaenda kuleta maendeleo ya Jimbo Jipya la Itwangi. Oktoba tunatiki kwa Azza Hillal Hamad na Dkt. Samia Suluhu Hassan na Madiwani wa CCM”, amesema Mayengo.

Naye Aliyekuwa Mtia Nia ya Ubunge Jimbo la Itwangi Mhandisi Sebastian Malunde, amewahimiza wananchi wa Itwangi kumpa miaka mitano mingine Rais Samia, akibainisha kuwa ndiye aliridhia kuundwa kwa Jimbo jipya la Itwangi baada ya kutengwa kutoka Jimbo la Solwa.

“Nimeisoma Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mkoa wa Shinyanga – imesheheni ahadi nyingi za kutatua changamoto za wananchi wa Itwangi kwenye sekta za afya, elimu, miundombinu, kilimo na umwagiliaji,” amesema.Mhandisi Sebastian Malunde

Aidha, amempongeza Rais Samia kwa kuendeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, akisema Tanzania sasa ni miongoni mwa nchi sita barani Afrika kati ya 54 zenye reli ya kiwango cha juu cha aina hiyo, jambo linalochochea uchumi wa Taifa.

Mhandisi Malunde amewaomba wananchi kumpigia kura Dkt. Samia, Mhe. Azza Hillal na madiwani wote wa CCM ili utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa kipindi cha 2025-2030 usikwame kutokana na changamoto za kisiasa.
Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, ambapo Watanzania watawachagua madiwani, wabunge na Rais.

TAZAMA PICHA MATUKIO YALIYOJIRI

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Itwangi – Picha na Kadama Malunde

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Itwangi

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Itwangi

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akiwanadi na kuwaombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad (kulia)na Mgombea Udiwani Kata ya Didia Richard Luhende.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi.


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akiwaombea kura wagombea udiwani kata za Jimbo la Itwangi
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akiwaombea kura wagombea udiwani kata za Jimbo la Itwangi

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akiwaombea kura wagombea udiwani kata za Jimbo la Itwangi

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi.


Mgombea Ubunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mzamva akiomba kura za Rais Dk Samia Suluhu Hassan, na Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi


Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM Taifa, Edwin Peter Nyakanyenge akimuombea kura Mgombea wa Ubunge Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Ndg. Edward Ngelela akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Jimbo la Itwangi

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Vijijini Ndg. Ernestina Richard akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Jimbo la Itwangi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Ndg. Edward Ngelela




Abiria kwenye Treni iliyopita eneo la Mkutano wa Kampeni akionesha Bango la Oktoba Tunatiki


Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akimuombea Mgombea Urais wa CCM,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad na Madiwani wote wa CCM.