Dkt. Mwinyi Azindua Kampeni za CCM Zanzibar kwa Kishindo – Global Publishers



ZANZIBAR-Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Septemba 14,  2025 amezindua rasmi kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika Uwanja wa Mnazi Mmoja, Mjini Magharibi.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameahidi kuendeleza kasi ya maendeleo kwa kuweka mkazo katika amani, elimu, afya, kilimo, ajira kwa vijana, miundombinu na uwezeshaji wananchi kiuchumi.